BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
KOCHA Mkuu wa Simba, Dylan Kerr ametoa programu maalumu kwa kila mchezaji wake ndani ya kikosi hasa wakati huu wa mapumziko ili watakaporudi wawe fiti tofauti na walivyokuwa kwenye mechi za mwisho za Ligi Kuu Bara msimu huu.


Nahodha wa Simba, Musa Mgosi, alisema kuwa programu hiyo ya mazoezi ni ngumu kwani inamlazimu kila mchezaji kuwa makini na kazi yake kwani hakuna muda tena wa kuendekeza mambo ya starehe.

"Unajuwa wachezaji wengi kipindi hiki cha mapumziko wanachukulia kama kipindi cha kufanya starehe lakini kocha ametupa programu yake na hiyo ni kwa kila mchezaji. Ni nzuri kwasababu inatuweka fiti ili ligi ikianza tuwe tayari kwa mapambano. Binafsi nimefurahishwa na hii programu kwani inaniweka imara zaidi.

"Alitueleza kuwa ligi ikianza itakuwa ngumu, ili tuweze kwenda na kasi hiyo ni lazima tujitume na kujitoa maana pia kuna usajili utafanywa hivyo timu nyingi zinaweza kuwa imara zaidi ya hapo awali na mazoezi hayo aliyotuachia ni kuendana na programu yake atakapoanza kazi hiyo," alisema Mgosi.


Mgosi alienda mbali kwa kusema kuwa mashabiki wengi humnyooshea vidole yeye hasa pale ambapo timu inapata matokeo mabaya lakini matokeo mengine yanakuwa nje ya uwezo wao.

Post a Comment

 
Top