BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Blida, Algeria
KATIKA kuonyesha kuwa aliridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na kikosi kilichoanza kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Algeria uliopigwa katika dimba la Taifa jijini Dar Es Salaam, kocha wa Stars Charles Mkwasa leo amepanga kikosi kile kile bila kufanya mabadiliko yoyote.

Stars itakayoingia dimbani majira ya saa 3:15 usiku kwa saa za Afrika Mashariki kuumana na Mbweha hao wa Jangwani, inatarajiwa kutumia mfumo ule ule wa kushambulia kwa kasi kwavile wanahitaji ushindi ili wafanikiwe kuwatoa Algeria.


Katika kikosi hicho Mkwasa amewaondoa katika orodha ya wachezaji wa akiba kiungo wa Simba Said Ndemla na Mrisho Ngassa huku Salum Telela na Jonas Mkude wakipewa nafasi zao.

Wachezaji wa akiba ni:
1. Aishi Manula
2. Mohamed Hussein 'Tshabalala'
3. Salim Mbonde
4. Salum Telela
5. Jonas Mkude
6. Simon Msuva
7. John Bocco
8. Malimi Busungu

Post a Comment

 
Top