BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ tayari kimewasili Addis Ababa nchini Ethiopia leo alfajiri kikiwa na wachezaji 18 pamoja na viongozi tayari kwa mashindano ya Kombe la Chalenji yatakayoanza kutimua vumbi kesho Jumamosi nchini humo.

Kilimanjaro Stars inayonolewa na Kocha Mkuu Abdallah Kibadeni, akisaidiwa na kocha msaidizi Juma Mgunda, imepangwa kundi A, ikiwa na wenyeji Ethiopia, Rwanda na Somalia.


Wachezaji waliosafiri na timu hiyo ni magolikipa Ally Mustafa na Aishi Manula, walinzi Shomari Kapombe, Kessy Ramdhan, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Salim Mbonde na Kelvin Yondani.

Wengine ni viungo Himid Mao, Salum Abubakar, Jonas Mkude, Salum Telela na Said Ndemla, huku safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Malimi Busungu, Elias Maguri, Simon Msuva, Deus Kaseke na nahodha John Bocco.

Stars itacheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Somalia siku ya Jumapili katika Uwanja wa Addis Ababa.

Post a Comment

 
Top