BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
TIMU ya Taifa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars leo imeibutua Somalia kwa mabao 4-0 huku washambuliaji Elias Maguli na John Bocco kila mmoja akifunga mabao mawili na kuiwezesha Stars iibuke na ushindi huo katika mechi yake ya kwanza tu ya michuano ya Chalenji inayoendelea nchini Ethiopia.


Bocco ndiye aliyekuwa wa kwanza kuiua Somalia kwa bao lililotokana na mkwanju wa penati katika dakika ya 11 kabla Maguli hajatupia la pili katika dakika ya 17

Kipindi cha pili Bocco na Maguli tena walirudi nyavuni safari hii Maguli akitingisha nyavu kwenye dakika ya 53 ambapo dakika tatu tu baadae Bocco akafunga kitabu cha mabao katika mchezo huo kwa bao la nne.

Stars chini ya Abdallah Kibadeni inahitaji ushindi mwingine ili kusonga mbele na katika mchezo unaofuata itakutana Rwanda mechi itakayopigwa Jumanne.Kikosi cha Kibadeni kipo Kundi A na timu za Ethiopia, Somalia na Rwanda.

Post a Comment

 
Top