BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
KOCHA wa zamani wa Taifa Stars, Mart Nooij amesaini mkataba wa kuifundiha timu ya St George ya  Ethiopia baada ya kufikia makubaliano na uongozi wa timu hiyo.

Nooij alisitishiwa mkataba wake na Shirikisho la Soka nchini (TFF) Juni mwaka huu baada ya kufungwa na Uganda katika mechi ya kufuzu kwa michuano ya Chan na sasa timu hiyo inafundishwa na Boniface Mkwasa.


Nooij amewahi kuifundisha timu hiyo miaka ya nyuma kabla ya kutua Stars na amekuwa ni kocha anayekubalika na mashabiki wa timu hiyo ya Ethiopia.

"Nooij anakuja kufundisha kwetu na tayari amemalizana na viongozi ni kocha mzuri tofauti na anavyodhaniwa. Alicheza mechi 30 na alipoteza moja pekee wakati huo anaifundisha.

"Anakubalika na viongozi pamoja na mashabiki, tulishangazwa Tanzania walipomuacha, Nooij ni kocha mwenye mafanikio na heshima kubwa katika soka,'' alisema kiongozi huyo.

Nooij (61) anatarajia  kutangazwa muda wowote kuanzia sasa kuwa kocha mkuu wa St George baada ya kumaliza taratibu zote.

Post a Comment

 
Top