BOIPLUS SPORTS BLOG

RAIS wa zamani wa Barcelona Juan Laporta amedai kamwe klabu hiyo haitathubutu kumuuza nyota wake wa kimataifa wa Argentina Lionel Messi, lakini akakiri kuwa Neymar anayewaniwa na Manchester United anaweza akauzwa siku za usoni.

Laporta amesema Messi ni kama sehemu ya nembo ya klabu hivyo si rahisi kupigwa bei lakini akasema katika kutunisha mfuko wa timu, mchezaji kama Neymar anaweza akauzwa mbele ya safari.


Rais huyo wa zamani wa Barcelona aliyeiongoza timu hiyo kati ya mwaka 2003 na 2010, alikiri kuwa katika kipindi hicho alizipiga chini ofa nyingi zilizomtaka mshindi huyo wa mara wa tuzo za Ballon d'Or.

Rais wa zamani wa Barcelona Joan Laporta amedai kamwe Lionel Messi hawezi kuondoka Barcelona
Laporta amesema mshindi huyo wa Ballon d'Or ni kama ya nembo ya Barcelona


Ingawa amesema Messi kamwe hataondoka Barcelona, lakini amesema Neymar anaweza akauzwa siku za usoni kwavile mazingira ya kiuchumi yanaweza yakachangia Barcelona kumuuza Neymar

Neymar mwenye umri wa miaka 23 amekuwa akiwindwa na Manchester United kwa zaidi ya miezi 12 iliyopita.


Post a Comment

 
Top