BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
MSHAMBULIAJI wa Simba, Raphael Kiongera raia wa Kenya amefunga mabao 11 katika msimu wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) lakini mabao hayo yameshindwa kuisaidia timu ya KCB kubaki kwenye ligi hiyo baada ya kukubali sare ya bao 1-1 na Western Stima.

Kiongera alipelekwa kwa mkopo katika timu hiyo aliyokuwa akiichezea kabla ya kutua Simba baada ya kupata majeraha ya goti na kufanyiwa upasuaji ambapo amecheza mechi 17 pekee. Mechi ya mwisho Kiongera hakucheza na ametoa sababu kuwa alikuwa na kadi tano za njano hivyo isingekuwa rahisi kwake kucheza kutokana na kanuni za ligi ya hiyo.


"Nilianza kucheza ligi ya huku katikati ya msimu, KCB haijaweza kubaki kwenye ligi labda ilikuwa ni mipango ya Mungu tu ila tulipambana kwa kadri tuwezavyo lakini haikuwa bahati yetu kubaki kwenye ligi. Mechi ya mwisho sikucheza kwasababu nilikuwa na kadi tano za njano," alisema Kiongera.

Kwasasa kitu pekee anachokisubiri Kiongera ambaye alikuwa Mchezaji Bora wa Agosti kwenye ligi ya KPL ni kurejea Simba kuja kumalizia mkataba wake uliobaki ambao unamalizika Juni mwakani. Gor Mahia ndiyo imetwaa ubingwa wa KPL kwa mara ya tatu mfululizo huku straika wao Jesse Were akiibuka Mfungaji Bora wa ligi hiyo.

Post a Comment

 
Top