BOIPLUS SPORTS BLOG

LICHA ya kuibuka mshindi wa ligi kuu ya Uingereza msimu uliopita ,Chelsea wamepata hasara ya dola milioni 34.9.

Kwa mujibu wa vitabu vya hesabu vilivyowasilishwa kwa mhasibu zinazofuatia makubaliano ya usawa wa fedha katika kandanda
Financial Fair Play (FFP), Chelsea inayomilikiwa na bilionea mrusi Roman Abramovich ilitangaza mapato ya pauni milioni 314.3, ikiwa ni hasara ya takriban pauni milioni 23.1 ikilinganishwa na mwaka wa 2013-14 ilipotangaza faida ya pauni milioni 319.8.
Matokeo hayo bila shaka yataibua maswali mengi kufuatia mwanzo mbaya katika ligi ya msimu huu ambapo the Blues wamesalia katika nafasi ya 15 .

Pia wadadisi wanahoji iwapo tangazo hilo litaibua wasiwasi kuhusu ushiriki wa Chelsea katika kombe la mabingwa barani Ulaya msimu huu.

Yamkini hasara hiyo ilitokana na kushindwa kwa klabu hiyo katika mkondo wa kwanza wa ligi ya mabingwa msimu uliopita na Paris Saint-Germain.

Chelsea ilitangaza faida kubwa zaidi ya pauni milioni 18.4 mwezi Novemba 2014 ya kwanza ya kiasi kama hicho kuwahi kutangazwa tangu bwenyenye huyo mrusi kukinunua klabu hicho mwaka wa 2003.Hayo ni ndwele, Chelsea inasema kuwa inatarajia kutangaza faida msimu huu baada ya kuandikisha mkataba wa pauni milioni 40 na kampuni ya kutengeneza magurudumu ya Yokohama.

Mwenyekiti wa Chelsea Bruce Buck ametangaza kuwa kuimarika kwa mgao wa fedha kwa vilabu vinavyoshiriki ligi ya mabingwa unatarajiwa kuisaidia The blues kupata faida msimu huu.

Post a Comment

 
Top