BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Christian Simba
MANCHESTER United imeitandika West Brom bao  2-0 lakini ushindi huo haujawasaidia kupanda kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England.

United inaendelea kushika nafasi ya nne huku Leicester City, Arsenal na Manchester City zikiendelea kuwa juu.

Magoli yote ya United yalikuja kipindi cha pili kupitia kwa kinda anayekuja juu Jesse Lingard kunako dakika ya 52 na Juan Mata aliyefunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 90.


Matokeo mengine ya mechi za Ligi Kuu zilizochezwa Jumamosi ni:
AFC Bournemouth 0 - 1 Newcastle United
Leicester City 2 - 1 Watford
Manchester United 2 - 0 West Bromwich Albion
Norwich City 1 - 0 Swansea City
Sunderland 0 - 1 Southampton
West Ham United 1 - 1 Everton

Post a Comment

 
Top