BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER City wakiwa kwenye uwanja wao wa Etihad wamechukua kipigo kitakatifu kutoka kwa Liverpool katika mchezo mkali wa Ligi Kuu nchini Uingereza ulioshuhudia nyavu zikitikisika mara tano.Hadi dakika ya 32 tayari Liverpool iliyoibuka na ushindi wa 4-1, ilikuwa mbele 3-0 kwa mabao ya Eliaquim Mangala aliyejifunga dakika ya 8, Philippe Coutinho dakika ya 23 na Roberto Firmino dakika ya 32.

Sergio Aguero akicheza mchezo wake wa kwanza baada ya kuwa majeruhi kwa wiki sita, akaifungia Manchester City bao pekee dakika ya 44 na kufanya timu hizo ziende mapumziko matokeo yakiwa 3-1.Beki wa kati wa Liverpool Martin Skrtel akahitimisha kwa bao la dakika ya 81 na kumfanya kocha Jurgen Klopp aanze kuamini kuwa sasa lolote linaweza kutokea katika mbio za kusaka taji la Premier League.

Post a Comment

 
Top