BOIPLUS SPORTS BLOG

REAL Madrid imefufua upya matumaini kwenye mbio za kuwania kutwaa taji la ligi kuu nchini Hispania 'La Liga' baada ya leo kuifunga Eibar iliyokuwa nyumbani kwa mabao 2-0. Mchezo huo ulichezwa  kwenye uwanja wa Ipurua.

 Winga Gareth Bale aliifungia Real Madrid bao la kwanza kwa kichwa katika dakika ya 43 akimaliza vema krosi ya Luca Modric. 

Bao hili lilikuja baada ya dakika nyingi za Madrid kumiliki mpira lakini wakakosa mipango mizuri ya kulifikia lango la wenyeji Eibar.

Madrid waliotoka kupokea kipigo cha mabao 4-0 nyumbani walipoikaribisha Barcelona, bado imeonyesha kukosa maelewano mazuri kwenye eneo la kiungo.

Kipindi cha pili Eibar walicharuka na kulifikia lango la Madrid mara kadhaa lakini bahati haikuwa yao kwani Christiano Ronaldo aliipatia Madrid bao la pili katika dakika ya 81  kwa mkwaju wa penati baada ya Lucas Vasquez kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari.

Post a Comment

 
Top