BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Blida, Algeria.

STRAIKA wa Stand United na Taifa Stars, Elius Maguli amesema kuwa kuitwa kwake na Kocha wa Stars, Boniface Mkwasa kuna maana kubwa na kwa vile kocha huyo amekubali kuwa ana uwezo wa kuichezea timu hiyo.

Maguli amesema kuwa mafanikio yake hayo yanatokana na kujituma uwanjani "Napenda kufunga kila ninapopata nafasi, nilitumia vema nafasi niliyoipata na ninategemea kufanya hivyo kila nipatapo nafasi, nashukuru kocha Mkwasa ameona kama nina uwezo wa kuichezea timu yake," 


Maguli anaongoza kwa magoli kwenye Ligi Kuu Bara akiwa na mabao tisa juzi Jumamosi aliisaidia Starskuifungia bao moja kati ya mawaili waliyopata huku moja likifungwa na Mbwana Samatta katika matokeo ya sare ya bao 2-2 dhidi ya Algeria mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 nchini Russia.

Tayari kiwango alichokionyesha Maguli kimeanza kuzitoa udenda baadhi ya timu ikiwemo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga pamoja na Mabingwa wa Afrika TP Mazembe ambapo vigogo hao wameanza kufuatilia nyendo za Maguli.

Post a Comment

 
Top