BOIPLUS SPORTS BLOG

AMA kweli 'La kuvunda halina ubani', mchezaji mmoja wa kikosi cha kwanza cha Chelsea amemwambia mtangazji wa BBC Radio 5 Live, Larry Richardson kuwa ni bora timu ifungwe kuliko kushinda kwa ajili ya Jose Mourinho.


Hatma ya kocha wa Chelsea Jose Mourinho imezidi kuwa mashakani baada ya kipigo cha 3-1 kutoka kwa Jumamosi ambapo Philippe Coutinho alifunga mara mbili ndani ya Stamford Bridge kikiwa ni kipigo cha sita kwa mabingwa hao watetezi katika mechi 11 za Premier League msimu huu.

Kocha huyo wa Chelsea alikingiwa kifua na tajiri wa timu Roman Abramovich mwezi uliopita, lakini tangu kipindi hicho timu haijaimarika huku wachezaji wakionekana wako chini ya kiwango chao.

Akizungumza Jumapili asubuhi, Richardson akasema: "Wacha nikuambie kuhusu mambo ya ndani ya Chelsea.

"Taarifa yangu inakuja kupitia mchezaji mmoja wa kikosi cha kwanza wa Chelsea.

"Nimeambiwa kuyumba kwa uhusiano wa Mourinho na wachezaji wake ndio msingi wa matatizo yote. 

Wanakerwa na namna anavyowaandama baadhi yao, uhusiano wake mbaya na wachezaji na hasa Eden Hazard unaididimiza timu.

"Mchezaji mmoja amethubutu kusema ni bora wafungwe kuliko kumpa ushindi Mourinho."

Post a Comment

 
Top