BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
WINGA Brian Majegwa raia wa Uganda imedaiwa kuwa yupo nchini tayari kwa ajili ya kumalizana na Simba baada ya Azam kuachana naye huku ikielezwa Majegwa ametua kwa siri kubwa.

Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam leo zilieleza kuwa Majegwa atasaini mkataba wa miaka miwili na Wekundu hao wa Msimbazi kama watafikia makubaliano yao ya mwisho ambapo tayari mazungumzo ya awali yalifanikiwa kwa asilimia kubwa.Chanzo cha habari kutoka Simba kimeiambia BOIPLUS kuwa mchezaji huyo kama watamalizana mapema basi huenda kesho atakuwepo kwenye mazoezi ya timu hiyo na kama ikishindika kumalizana kwa wakati basi ataanza mazoezi hayo baadaye.

''Bryan yupo jijini Dar es Salaam tayari, ishu yake na Azam nafikiri imemalizika hivyo anaweza kusaini mkataba na Simba muda wowote kwani huyo ana asilimia kubwa ya kujiunga na sisi maana tangu usajili mkubwa tulikuwa tunamuhitaji.

''Anakuja kwetu kama mchezaji huru kwani Azam walimuacha mpaka suala lake lilifika TFF kwasababu hawakumlipa fedha zake za kumvunjia mkataba wake,'' alisema kiongozi huyo.

Kwa upande wa mshambuliaji wao Mkenya, Raphael Kiongera yeye atajiunga na Simba mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Challenji ambapo yeye amechaguliwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Kenya.''Sijatumiwa tiketi na Simba bado na vile vile naenda Ethiopia labda kama watanitumia hapo baadaye ndiyo nitajua nakuja lini kujiunga na Simba,'' alisema Kiongera.

Hata hivyo habari kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa kuna mchezaji kutoka Rwanda amekuja kwa ajili ya majaribio ambapo ameletwa na wakala aliyemleta Papa Niang.

Post a Comment

 
Top