BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
WINGA Brian Majwega leo Jumatatu huenda ataondoka nchini kurudi kwao Kampala, Uganda kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kukabiliwa na matatizo ya kifamilia.

Simba jana Jumapili iliingia kambini visiwani Zanzibar kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara huku ikimuacha Majwega jijini Dar es Salaam ambapo mechi yao ya Desemba 12 itakuwa dhidi ya Azam FC.


Habari zilizopatikana jijini hapa zinasema kuwa Majwega ambaye aliomba kufanya mazoezi na Simba wakati akisubiri tatizo lake na timu yake ya Azam Fc litatuliwe na Shirikisho la Soka nchini (TFF) atajiunga na Simba baada ya kumaliza matatizo yake hayo.

Majwega aliomba kuwepo Simba ili kulinda kiwango chake cha soka huku akiweka wazi kuwa hataki tena kuichezea Azam ambayo bado inadai kuwa ni mchezaji wao halali kwani ana mkataba nao.

''Majwega yeye hajaenda Zanzibar kwani ana matatizo ya kifamilia na huenda kesho ataondoka kurudi kwao kwenda kutatua matatizo hayo, suala lake bado halijaisha na lipo TFF hivyo tutajua hatima ya hili hapo baadaye,'' alisema kiongozi huyo.

BOIPLUS inafahamu kwamba Simba wanamuhitaji Majwega kwa udi na uvumba na wanachokisubiri kwasasa ni uamuzi wa TFF juu ya mgogoro wao wa kimkataba kati ya winga huyo na Azam.

Endapo TFF itaamuru kuwa mchezaji huyo yupo huru kusajiliwa na timu yoyote basi ni wazi kuwa atasaini mkataba Simba.

Post a Comment

 
Top