BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Christian Simba
HAKUNA Wayne Rooney wala Anthony Martial lakini bado hakuna tatizo, Manchester United wanavuna pointi tatu muhimu.

Wakicheza ugenini dhidi ya Watford katika mchezo wa ligi kuu Uingereza, United wanaibuka na ushindi wa bao 2-1, ushindi uliokuja kwa mbinde baada ya wenyeji kutawala sehemu kubwa ya mchezo.


Alikuwa ni Memphis Depay ndiye aliyeipatia United bao la kuongoza dakika ya 11 baada ya kuunganisha pasi nzuri ya Ander Herrera.

Troy Deeney aliizawazishia Watford kwa penalti ya dakika ya 87 lakini ni Deeney huyo huyo aliyeipa ushindi Manchester United baada ya kujifunga dakika ya 90 kufuatia krosi iliyopigwa kwenye kisanduku cha sita na Bastian Schweinsteiger.


WATFORD (4-4-2): Gomes 6, Nyom 5 (Paredes 69, 6), Cathcart 6, Britos 6, Anya 6, Capoue 7.5, Watson 5.5, Abdi 6.5, Deeney 7, Jurado 4.5 (Ake 45, 6), Ighalo 6.5

MANCHESTER UNITED (4-2-3-1): De Gea 6.5, Young 7, Jones 7.5 (McNair 69, 6), Smalling 7, Blind 6, Schneiderlin 8.5, Schweinsteiger 7.5, Mata 6.5 (Pereira 79, 6), Herrera 6.5 (Rojo 25, 5.5), Lingard 7, Depay 8

Post a Comment

 
Top