BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
MBEYA CITY ipo kwenye mchakato wa mwisho wa kumrudisha mchezaji wao Deo Julius ambaye anakipiga katika timu ya Kagera Sugar inayoshiriki Ligi Kuu Bara.

Kagera Sugar ilimsajili mchezaji huyo kutokea City baada ya kushindwa kumpa mkataba mpya baada ya ule wa awali kumalizika na hivyo kuuamua kujiunga Kagera kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Deo Julius


Mchezaji huyo ambaye kwasasa yupo jijini Mbeya ameiambia BOIPLUS kuwa tayari mazungumzo ya pande mbili Mbeya City na Kagera Sugar ya kuvunja mkataba wake yanaendelea vizuri na huenda akasaini mkataba muda wowote kuanzia sasa.

Deo amesema kuwa kikubwa anachokiangalia ni fedha na wala hachagui wapi afanye kazi kwani mpira ndio ajira yake hivyo haoni tatizo kurejea kwenye timu yake ya zamani.

''Ni kweli nitarudi Mbeya hapa nasubiri viongozi wa Mbeya City wamalizane na viongozi wangu wa Kagera maana kule nina mkataba. Sina tatizo kurudi City kwani ninachokiangalia sasa ni masilahi na kucheza soka ndiyo ajira yangu,'' alisema Deo

Post a Comment

 
Top