BOIPLUS SPORTS BLOG

STRAIKA wa Azam FC, Hamis Mcha, amesema kuwa kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Herous' inayojiandaa na michuano ya Kombe la Chalenji ni neema kwake kwani hapati nafasi kwenye kikosi chake kinachoshiriki Ligi Kuu Bara.


Mcha ni miongoni mwa wachezaji sita walioitwa kutoka Azam na kwenda kuisaidia Zanzibar Herous kwenye michuano hiyo inayoanza Novemba 21 jijini Addis Ababa, Ethiopia akiwemo Mwadin Ally, Ame Ally, Agrey Morris, Ismail Khamis na Mudathir Yahya.


Mcha amesema kuwa alikuwa na uchu wa kucheza hasa baada ya kupoteza namba kwenye kikosi chake hivyo kuitwa kwake Stars kunampa faraja ya kurejesha makali yake na kumshawishi kocha wake Stewart Hall kumrejesha kikosini. 

"Huu ni muda mzuri kwangu kutumia nafasi hii kurejesha kiwango changu na kupata namba kwenye kikosi cha Azam, na hiyo itanisaidia kuendana na jinsi kocha anavyotaka maana lengo langu ni kucheza kikosi cha kwanza," alisema Mcha.


Kocha Mkuu wa Zanzibar Herous Hemed Morocco alisema "Wachezaji tuliowaita ni wale wale wa siku zote ila tumeongeza wachache tu kwani wengine ni majeruhi hivyo tusingeweza kuita tu, naamini nikijiunga nao nitakuta wapo fiti,".

Post a Comment

 
Top