BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
KOCHA wa zamani wa JKT Ruvu, Felix Minziro leo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha Panone FC ya jijini Moshi.

Baada ya kusaini mkataba huo na matajiri hao wa Moshi ambao wanashiriki Ligi Daraja la Kwanza, Minziro ataanza kazi yake rasmi Jumatatu ya wiki ijayo.


Mwenyeki wa Bodi ya Wakurugenzi wa Panone, Alhaji Mohamed Karia kushoto akimkabidhi Felix Minziro mkataba


Msemaji wa klabu hiyo, Kassim Mwinyi ameiambia BOIPLUS kuwa kila kitu kimemalizwa leo na taratibu za usajili zitaanza kufanywa wiki ijayo chini ya Minziro ambapo timu hiyo inatarajia kutema wachezaji saba na kusajili kumi katika dirisha dogo la usajili unaoendelea.

''Minziro tumemalizana naye na atakuwa kwetu kwa mwaka mmoja, wiki ijayo ndio ataanza kazi rasmi. Kuhusu usajili tuna nafasi tatu ambazo hatukujaza wakati wa usajili mkubwa hivyo tutaacha wachezaji saba na kusajili kumi.

''Tunaita wachezaji 16 kwenye majaribio kutoka timu mbalimbali za mikoa tofauti na wale ambao kocha ataona wanamfaa watasajiliwa tayari kwa kuanza kufanyakazi na Panone,'' alisema KassimMinziro aliacha kuifundisha JKT Ruvu baada ya timu hiyo kupata matokeo mabaya mfululizo ambapo nafasi yake ilichukuliwa na kocha Abdallah Kibadeni ambaye amefanikiwa kuibadilisha timu hiyo na kuiondoa mkiani ambako ilikuwa imekaa kwa kipindi kirefu.

Post a Comment

 
Top