BOIPLUS SPORTS BLOG

KIUNGO  wa Simba, Jonas Mkude amesema kuwa anaamini timu yao ni bora na ina nafasi kubwa ya kutwaa ana imani kubwa ya ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Mpaka sasa Simba inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 21, Azam ikiongoza kwa pointi 25, Yanga wana pointi 23 huku Mtibwa Sugar wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 22.


Mkude amesema kuwa Simba kwasasa ipo vizuri na kila mchezaji anajituma kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri na kupata nafasi ya kushiriko michuano ya kimataifa ambayo hawajashiriki kwa zaidi ya miaka miwili sasa.

“Ukiangalia kwenye msimamo wa ligi hatupo vibaya bado nafasi ipo vizuri na kocha anapigana kuhakikisha anaiweka sawa zaidi. Wachezaji wote tuna lengo la kushika nafasi bora za juu hasa kutwaa ubingwa,'' alisema Mkude.

Simba tayari wameanza mazoezi ya ufukweni ambapo Mkude hajajiunga na kikosi hicho kwani yupo kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Kilimanjaro Stars inayojiandaa na michuano ya Kombe la Challenji inayoanza keshokutwa Jumamosi jijini Adis Ababa, Ethiopia.

Mkude alikuwemo kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichoondolewa kwenye mbio za kuwania kushiriki Kombe la Dunia 2018 na Algeria kwa kufungwa bao 7-0 huku mchezo wa awali ukiisha kwa sare ya bao 2-2.

Post a Comment

 
Top