BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Christian Simba
ZIKIWA zimebaki siku nne kuelekea mchezo wa mahasimu wakubwa wa soka la Hispania, El Classico inayowakutanisha miamba yasoka Real Madrid na Barcelona, Lionel Messi ameanza mazoezi jana Jumatatu tayari kwa mechi hiyo.

Habari hizi sio za kufurahisha kwa mashabiki wa Real Madrid ambao wasingependa kukutana na Barcelona hii yenye Lionel Messi ndani huku pia Ivan Rakitic naye akitajwa kuwa fiti baada ya kupona majeraha yake.


Messi ambaye alikaa nje ya uwanja, tangu alipoumia mwishoni kwa mwezi Septemba Barcelona ikicheza dhidi ya Las Palma’s anatarajiwa kucheza katika mchezo huo utakaopigwa Santiago Bernabeu uwanja wa Real Madrid Jumamosi hii.

Barcelona haikuonekana kuyumba sana baada ya kukosekana kwa nyota huyo, ujio wake ni habari za faraja kwa mashabiki wa Barca na kocha wao Luiz Enrique ambao sasa watakua wanaombea kuona mchezaji huyo anarudia kiwango chake pamoja na kuwa alikua nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili.

Post a Comment

 
Top