BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
LICHA ya kuwa akili na masikio yao yanawaza mechi ya kesho dhidi ya Taifa Stars na Algeria lakini winga wa Yanga, Simon Msuva hajasahau majukumu na malengo yake katika kikosi cha Yanga na kutamka kuwa atarudi kwenye kikosi hicho akiwa imara zaidi.

Msuva amesema kuwa kikubwa kwasasa ni kuhakikisha Stars wanaifunga Algeria kesho kwenye mechi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018 lakini pia ni kuhakikisha wachezaji wa Yanga wanatetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara.


Msuva ambaye ni Mfungaji Bora wa msimu uliopita alisema ''Mazoezi tunayopewa hapa Stars ni mazuri mno kiasi kwamba yataturahisishia tutakapojiunga na timu zetu kujiandaa na mechi za Ligi Kuu. Kwa hakika tumeiva na lengo letu kwa upande wa Yanga ni kutetea ubingwa tu.

''Nafikiri mechi ya kesho na Algeria ni kujitoa zaidi kuhakikisha tunapata ushindi mnono tukiwa nyumbani. Hii ni mechi kubwa na ngumu ila tutafanya vizuri kutokana na maandalizi tuliyoyafanya,'' alisema Msuva.

Yanga iliyo chini ya Kocha Hans Pluijm ndiyo timu pekee ambayo imeanza mazoezi yake jana kwa ajili ya maandalizi ya ligi hiyo ambapo wao wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 23 huku Azam wakiwa kileleni kwa pointi 21.

Post a Comment

 
Top