BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
STRAIKA wa JKT Ruvu, Saady Kipanga amesema kuwa timu yao kamwe haiwezi kushuka daraja huku akitamba kuwa kwasasa kazi imeanza rasmi baada ya kugundua mapungufu yao ambayo yanafanyiwa kazi.

JKT Ruvu ni timu ambayo misimu yote ya Ligi Kuu Bara huanza vizuri lakini msimu huu umekuwa mbaya kwao kwani walianza vibaya na kujikuta wakishika mkia muda mrefu ingawa sasa wamejinasua mkiani.Tangu timu hiyo akabidhiwe kocha Abdallah Kibadeni na Mrage Kabange imekuwa na mabadiliko makubwa ambayo yameanza kuwapa matumaini mapya wachezaji wa timu hiyo ya jeshi.

Akizungumza na BOIPLUS, Kipanga alisema kuwa kadri siku zinavyosonga mbele wanazidi kuimarika  na hawataweza kushuka kwani kikosi chao kipo imara tofauti na walivyoanza.''Hatushuki daraja ingawa tulianza vibaya, mpira uko hivyo lakini tunabaki kusema watashuka wengine na sio sisi. Tumedhamiria na ndiyo maana tunafanya mazoezi mara mbili kwa siku,'' alisema Kipanga.

Kesho timu hiyo itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Chuo cha Biashara (CBE), mechi itakayochezwa Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top