BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Mrundi Suleiman Ndikumana amesema kuwa ukitaka kupata uhondo wa soka la beki wa Azam FC, Paschal Wawa basi achezeshwe nafasi ya kiungo mkabaji na si hiyo anayocheza kwasasa kwenye kikosi hicho cha Mabingwa wa Kombe la Kagame.

Hayo aliyazungumza hivi karibuni katika mahojiano maalumu kwamba Kocha wa Azam anapaswa kumtumia Wawa kwenye nafasi hiyo ambayo huimudu zaidi kuliko hiyo ya sasa.


"Namfahamu vizuri Wawa kwani nimecheza naye El Merreikh, anacheza nafasi mbili beki ya kati na namba sita, kwenye timu yetu ndiye mchezaji pekee tuliyekuwa tunamtegemea kwenye mechi ngumu kwamba atatubeba na kocha alikuwa anampanga kucheza kiungo mkabaji.

"Wawa ni mchezaji mwenye vurugu nyingi uwanjani hasa akicheza na mtu ambaye anamfahamu, yupo tayari apate kadi nyekundi lakini awe amewatoa mchezoni wapinzani wake, naamini Hall akimjaribu kumchezesha nafasi hiyo basi hataacha na atafurahia zaidi," alisema Ndikumana.

Seleman Ndikumana


Kwasasa Ndikumana ambaye pia ameitwa kikosi cha timu ya Taifa ya Burundi ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake wa miezi sita na timu ya Primeiro d'Agosto ya Angola ingawa kuna uwezekano mkubwa wa kumwongeza mkataba mwingine.

Post a Comment

 
Top