BOIPLUS SPORTS BLOG

CRISTIANO Ronaldo huenda atacheza mchezo wake wa mwisho wa nyumbani wa El Clasico ya La Liga Jumamosi ijayo ikiaminika kuwa ndoa yake na Real Madrid inaweza kufikia tamati mwezi Mei mwakani.


Daily Mail la Uingereza linaandika kuwa habari za ndani kutoka kwa klabu hiyo ya Hispania ambayo Ronaldo amekuwa akiitumikia tangu mwaka 2009, zinasema supastaa huyo wa Kireno hataichezea tena Real Madrid msimu ujao.

Habari hizo zinachagizwa na namna Real Madrid walivyoutosa uzinduzi wa filamu ya Ronaldo iliyozinduliwa London Jumatatu iliyopita.


Ronaldo anahusishwa kwa kiasi kikubwa na usajili wa kurejea tena Manchester United, klabu iliyoitumikia kwa mafanikio makubwa kabla hajajiunga na Real Madrid.

Post a Comment

 
Top