BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Blida, Algeria
MSHAMBULIAJI wa Free State ya Afrika Kusini na Taifa Stars, Mrisho Ngasa amesema kuwa ingawa anafurahia maisha ya soka nchini humo lakini kama atapata dili la kwenda kucheza soka Ulaya basi yupo tayari kuachana na klabu hiyo iliyomsajili kwa dola 150,000.

Kauli hiyo ameitoa baada ya kuonekana haridhishwi na mafanikio yake kisoka na hivyo kumfanya aanze kufikiria kutoka ndani ya nje hilo na kuangalia soka la kimataifa zaidi.

Mrisho Ngassa (kulia) akiwa na kikosi cha Taifa Stars


''Si kwamba Afrika Kusini maisha ni mabaya, maisha ni mazuri lakini naona bado si mwisho wa safari yangu, nikipata timu nje hasa nchi za Ulaya basi nitaangalia utaratibu wa kwenda kucheza huko," alisema Ngassa ambaye alisaini mkataba wa miaka minne na timu hiyo na aliwahi kufanya majaribio na West Ham ya Uingereza lakini hakufanikiwa kuichezea timu hiyo.

Kwa sasa Ngassa yupo na kikosi cha Stars kitakachoivaa Algeria hapo kesho kwenye mechi ya marudiano ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018, mechi ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Stars walitoka sare ya bao 2-2 hivyo wanatakiwa kupata ushindi wa bao 1-0 au sare ya bao 3-3.

Post a Comment

 
Top