BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
SHIRIKISHO la soka duniani FIFA limetaja majina ya wanamichezo walioingia fainali kuwania tuzo mbalimbali za dunia ikiwemo mchezaji bora wa Dunia mwanaume, mchezaji bora wa dunia mwanamke, kocha bora wa soka la wanaume, kocha bora wa soka la wanawake na goli bora la mwaka.

Kwa upande wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia, FIFA Ballon d'Or  2015 kwa soka la wanaume, waliofanikiwa kuingia fainali ni Cristiano Ronaldo (Ureno/Real Madrid), Lionel Messi (Argentina/Fc Barcelona) na Neymar (Brazil/Fc Barcelona). 

Mchezaji bora wa Dunia kwa  upande wa wanawake walioingia fainali ni Carli Lloyd (USA/Houston Dash), Aya Miyama (Japan/OkayamaYunogo Belle) na Célia Šašić (Germany/1. FFC Frankfurt)

Walioingia fainali kwa upande wa kocha bora wa Dunia kwa soka la wanaume ni Pep Guardiola (Spain/ FC Bayern Munich), Luis Enrique Martinez (Spain/Fc Barcelona) na Jorge Sampaoli (Argentina/Timu ya taifa Chile)

Jill Ellis (USA/Timu ya taufa USA), Mark Sampson (Wales/Timu ya taifa ya Uingereza) na Norio Sasaki (Japan/Timu ya Taifa Japan) ndio walioingia fainali katika kinyang'anyiro cha kocha bora wa mwaka kwa soka la wanawake.

Kwa upande wa bao bora la mwaka, walioingia fainali ni Alessandro Florenzi (Italia/Roma), Wendell Lira (Brazil/Vila Nova) na Messi .
 Tuzo hizo zitatolewa Januari 11 mwakani jijini Zurich, Uswisi.

Post a Comment

 
Top