BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Dar
SIRI ya nidhamu bora ya straika wa TP Mazembe na Taifa Stars, Mbwana Samatta 'Poppa', inatokana na kazi ya jeshi waliyokuwa wakiifanya wazazi wake ambayo nidhamu ndiyo kila kitu na kwamba alipewa mtego wa kumlipa baba yake faini ya Sh 2,000 kila akikosa penalti.


Akizungumza mara baada ya kumpokea mtoto wao huyo aliyewasili leo akitokea Lubumbashi kuja nchini kujiunga na Taifa Stars, baba mzazi wa Samatta, Ally Pazi Samatta, amesema kuwa mafunzo ya kineshi waliyopitia wazazi wake ndiyo yalitoa mwongozo wa maisha ya Samatta.

"Mimi na mama yake tulikuwa makamanda wa polisi  kazi ambayo kwa kipindi hicho ilihitaji nidhamu ya hali juu ndiyo maana hata vijana wetu walilelewa hivyo, mbali na hilo mimi nilikuwa mchezaji wa Simba na Stars, hilo pia lilitosha kuwaongoza vijana wangu kujua nidhamu ya soka ili waweze kufika mbali nashukuru Mungu, limetimia kwa Samatta, ingawa wengine wameishia kucheza Ligi Kuu Bara," alisema Mzee Samatta.

Samatta akiwa na familia yake


Mzee Samatta alisema katika mambo aliyomsisitiza mwanaye kuyafanya ni pamoja na nidhamu na kumtanguliza Mwenyenzi Mungu kwa kila jambo.

"Samatta na kaka yake Mohammed Samatta ambaye anacheza Mgambo JKT, nimewawekea faini pale wanapoonyesha kukosa  nidhamu uwanjani kwa hiyo wamekuwa wakizingatia sana maelekezo hayo, siku moja niliwaambia mtu akikosa penalti anatakiwa kulipa Sh 2,000.

Mzee Samatta katikati akimpokea mwanae kulia


"Kusikia adhabu hiyo wote walicheka sana lakini nilipofafanua kuwa watalazimika kuleta nyumbani moja kwa moja bila kutuma sehemu yoyote hata kama Samatta atakuwa Mazembe itambidi asafiri kuja ndipo walipoona ugumu wa adhabu hiyo, lengo ni kuona wanakuwa makini kila siku", alisema Mzee Samatta.

Post a Comment

 
Top