BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
SHIRIKISHO la soka barani Afrika (CAF) leo limetangaza orodha ya wachezaji walioingia kwenye hatua ya 10 bora kwenye kinyang'anyiro cha kumtafuta mchezaji bora wa jumla wa Afrika pamoja na mchezaji bora wa Afrika kwa wanaocheza ndani.

Mtanzania Mbwana Samatta anayechezea TP Mazembe ya DR Congo ameingia kwenye hatua hiyo kwa mara ya kwanza huku akiwabwaga mastaa kibao katika mchujo huo.

Zifuatazo ni orodha mbili za wachezaji waliobaki kuwania tuzo hizo.

MCHEZAJI BORA WA AFRIKA
1. André Ayew (Ghana & Swansea)

2. Aymen Abdennour (Tunisia & Valencia)

3. Mudather Eltaib Ibrahim ‘Karika’ (Sudan & El Hilal)

4. Mohamed Salah (Egypt & Roma)

5. Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund)

6. Sadio Mané (Senegal & Southampton)

7. Serge Aurier (Cote d’Ivoire & Paris Saint Germain)

8. Sofiane Feghouli (Algeria & Valencia)

9. Yacine Brahimi ( Algeria & Porto)

10. Yaya Touré (Cote d’Ivoire & Manchester City)
MCHEZAJI BORA ANAYECHEZA AFRIKA
1. Abdeladim Khadrouf (Morocco & Moghreb Tetouan)

2. Baghdad Bounedjah ( Algeria & Etoile du Sahel)

3. Felipe Ovono (Equatorial Guinea & Orlando Pirates)

4. Kermit Erasmus (South Africa & Orlando Pirates)

5. Mbwana Aly Samatta (Tanzania & TP Mazembe)

6. Mohamed Meftah ( Algeria & USM Alger)

7. Mudather Eltaib Ibrahim ‘Karika’ (Sudan & El Hilal)

8. Robert Kidiaba Muteba ( DR Congo & TP Mazembe)

9. Roger Assalé (Cote d’Ivoire & TP Mazembe)

10. Zineddine Ferhat (Algeria & USM Alger)

Washindi katika nyanja zote watapatikana kwa kupigiwa kura na makocha au wakurugenzi wa ufundi wa timu za taifa ambazo ni wanachama wa CAF, na watatangazwa januari 7 mwakani.

BOIPLUS inamtakia kila la heri Samatta katika kinyang'anyiro hicho.

Post a Comment

 
Top