BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda, Lubumbashi
UKISTAAJABU ya Mussa basi utaona ya Firauni. Huwezi amini, ili upate bidhaa ndani ya duka la TP Mazembe linalofahamika kwa jina la 'TP Mazembe Boutique' basi kubali kupanga foleni. Idadi ya mashabiki wanaoingia dukani hapo kununua jezi na vifaa vingine ni kubwa na inafurahisha sana.

Duka hili lililo ndani ya uwanja wa Mazembe ni sehemu nyingine inayotuonyesha tofauti iliyopo kati ya timu hiyo na klabu nyingine za hapa Afrika. Mashabiki wa Mazembe wanaonyesha wazi mapenzi yao ya hali ya juu kwa timu yao. BOIPLUS ilifanya mahojiano na baadhi ya mashabiki dukani hapo na asilimia kuwa walikiri kuwa na jezi halisi zisizopungua kumi nyumbani kwao.

Tazama picha za matukio ndani ya duka hilo.


Fulana za TP Mazembe


Watu wa mataifa mbalimbali hununua bidhaa dukani hapo

Mwandishi wa BOIPLUS(kushoto) akiwa na Shaffih Dauda wa Clouds Media

Tiketi za kisasa kabisa ambazo mtazamaji huvaa mkononi
Post a Comment

 
Top