BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
STRAIKA Elius Maguli sasa ndiye gumzo kwa wachezaji wazawa na hiyo ni baada ya kuonyesha kiwango cha juu katika upachikaji wa mabao ambapo amefunga mabao tisa kwenye mechi za Ligi Kuu Bara lakini viongozi wake wa Stand United wamesema hawamuuzi mchezaji huyo kwenye klabu yoyote ya nchini.

Maguli kwasasa yupo kwenye kikosi cha timu ya taifa 'Taifa Stars' na Kilimanjaro Stars ambacho kitashiriki michuano ya Kombe la Challenji inayoanza Novemba 21 jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Yanga ndiyo klabu ya kwanza kuanza kummezea mate straika huyo aliyetemwa na Simba baada ya kocha wao mkuu, Dylan Kerr kutoridhishwa na kiwango chake na hivyo kuamua kuvunja mkataba ambapo alisajiliwa na Stand United ya Shinyanga chini ya Kocha, Patrick Leiwig.


Yanga walisema watakuwa tayari kumnyakuwa Maguli endapo ataamua kwa ridhaa yake kuvunja mkataba kwani wanaamini ni mchezaji mzuri anayeweza kuisadia timu yao kwasasa ambayo ina nyota kibao.

Wakati Yanga ikiwaza hivyo tayari TP Mazembe wameanza kufuatilia kiwango cha mchezaji huyo na wachezaji pekee watakaowaambia ukweli matajiri hao wa DR Congo ni Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.

Kocha Msaidizi wa Stand United, Athuman Bilali 'Billo' amesema kuwa "Tunasikia tu kwenye vyumbo vya habari kuwa Yanga wanamtaka Maguli lakini hatuwezi kumwachia kwa timu za hapa ni bora biashara ifanye na timu ya nje, pale Yanga wakimchukuwa Maguli nani atakaa benchi, kwani alivyokuwa Simba hawakumuona.

''Tuna malengo ya kukaa kwenye nafasi bora za juu na Maguli ni miongoni mwa wachezaji ambao watatuweka kwenye nafasi hiyo,  inauma sana kumwona mchezaji kama Abisalim Chidiebele alienda Coastal Union akiwa ndiye Mfungaji Bora wa timu yetu lakini kule ameshindwa kufanya vizuri kutokana na mfuo wa timu, Maguli aende wapi kwasasa," alisema Bilali.

Post a Comment

 
Top