BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
KILIMANJARO Stars imeingia hatua ya robo fainali baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Ethiopia katika mechi ya mwisho ya makundi iliyochezwa leo huku Kili Stars ikiongoza Kundi A ikiwa na pointi saba katika michuano hiyo ya Kombe ya Challenji.Bao la Kili Stars lilifungwa na winga Simon Msuva huku wenyeji wakipata bao la kusawazisha baada ya beki wa Kili Stars Salim Mbonde kujifunga wakati akiwa katika harakati za kuokoa hatari langoni mwao.

Katika mchezo wa awali uliozikutanisha Uganda dhidi ya  Burundi, Uganda ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Hivyo basi, Kili Stars itakutana tena na Ethiopia kwenye hatua ya robo fainali siku ya Jumatatu mchezo utakaopigwa kwenye Mji wa Addis Ababa.

Post a Comment

 
Top