BOIPLUS SPORTS BLOG

TAWI la Simba ya jijini Dar es Salaam lijulikanalo kwa jina la Simba Damu Fans ' SDF' leo lilifanya mkutano mkuu kwenye ofisi zao zilizopo Tabata Kimanga na kukubaliana kwa pamoja kufanya uchaguzi mkuu ifikapo Disemba 13 .


Akizungumza na BOIPLUS, Katibu Mkuu wa SDF, Severin Machilla 'Mwanakijiji' alisema mkutano mkuu umeamua kwa pamoja kuwa uchaguzi mkuu ufanyike mwezi ujao.

"Mkutano umemalizika kwa wanachama kukubaliana na ombi letu kamati ya utendaji la kuitisha uchaguzi mkuu kwa haraka, na kwamba kesho nitakwenda klabu kuwasilisha rasmi maombi yetu ya kufanya uchaguzi Disemba 13 kama ilivyoamuliwa na mkutano mkuu wa tawi" alisema Machilla

Uchaguzi huo utahusisha nafasi ya Mwenyekiti wa tawi na makamu wake pamoja na wajumbe wanne wa kamati ya utendaji. Nafasi za Katibu Mkuu, Afisa Mipango na Mhasibu hizi zitajazwa kwa kuteuliwa na kamati ya Utendaji itakayochaguliwa.

Viongozi waliopo madarakani sasa walishamaliza muda wao wa uongozi mwezi januari ila walipewa muda zaidi hadi wakamilishe zoezi la kusajili SDF kuwa tawi rasmi la Simba, baada ya kukamilisha zoezi hilo mapema mwezi Oktoba basi umeamua kuitisha uchaguzi.

Mambo ya 'Selfie' baada ya kukabidhiwa kadi za uanachama


Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa tawi hilo, Karim Boimanda aligawa kadi za uanachama wa Simba kwa wanachama wapya waliohudhuria mkutano huo.

Post a Comment

 
Top