BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kilichoondolewa na timu ya Taifa ya Algeria kwenye michuano ya kuwania kufuzu kwa kombe la Dunia 2018 na kwa jumla ya mabao 9-2 kimetua jijini Dar usiku huu majira ya saa 9 alfajiri kwa ndege ya shirika la ndege la Turkish Air.

BOIPLUS ilikuwepo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) na kushuhudia vijana hao wakishuka na sura za huzuni mno.

 Jambo pekee lililowafanya wachangamke kidogo ni pale walipokuta kikundi cha uhamasishaji kinachojulikana kwa jina la 'Taifa Stars Supporters' kikipiga ngoma, kuimba na kufungua shampeni kwa lengo la kuwaonyesha kuwa licha ya matokeo mabaya waliyoyapata nchini Algeria, bado Watanzania wapo pamoja nao.

Tazama picha za kikosi hicho kilipowasili.

Straika Mbwana Samatta 
Kocha Charles Mkwasa akiwa na Taifa Stars Supporters
Wazee wa 'kigoma' wakifanya mambo yao Airport
Mashabiki wa Stars wakiwa nje ya basi la timu hiyo kabla halijaondoka kuwapeleka wachezaji hotelini
Afsa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto kushoto Shomari Kapombe kushoto na John Bocco
Jonas Mkude kushoto na Mrisho Ngassa
Mmiliki na mwandishi wa mtandao wa BIN ZUBEIRY SPORTS-ONLINE, Mahamoud Zubeiry katikati akiteta jambo na Msemaji wa zamani wa Simba, Asha Muhaji
Post a Comment

 
Top