BOIPLUS SPORTS BLOGKocha wa Yanga, Hans Pluijm na kocha wa Simba,Dylan Kerr
SHINDANO la Nani Mtani Jembe linaloshirikisha timu ya Simba na Yanga kwa zaidi ya miaka miwili sasa imefutwa rasmi huku wadhamini wa timu hizo kongwe nchini, Kilimanjaro Lager wakiweka wazi kuwa mwaka huu shindano hilo halitafanyika kutokana na sababu zilizo ndani ya kampuni yao.

Meneja wa kinywaji hicho kilicho chini ya Kampuni ya Bia nchini (TBL), Pamela Kikuli amekiri kufutwa kwa shindano hilo kwa kile alichoeleza kuwa halipo kwenye mkataba wao wa udhamini kwa klabu hizo mbili bali ilikuwa ni kufanya promosheni ya kuitangaza bidhaa yao hiyo.

Alisema kuwa taarifa za awali ziliwafikia viongozi wa pande zote mbili ambao ni Simba na Yanga katika kikoa chao cha pamoja na kwamba kama shindano hilo lingekuwepo basi wangewaita tena ili kujadili kama kungekuwepo na maboresho ama kuwa vile vile.

"Viongozi wa Simba na Yanga wanajua kuwa hatutafanya kwa mwaka huu, tuliwaeleza kwenye kikao cha awali tulipokutana nao, shindano hili halipo kwenye mikataba yao ambayo tumewadhamini bali ni promosheni tu ya kutangaza bidhaa yetu, hivyo sababu za kutofanya mwaka huu zipo ndani ya kampuni yetu," alisema Pamela.

TBL imeendesha shindano hilo mara mbili ambazo zote Simba imekuwa ikiibuka kidedea kwa kuifunga Yanga, mwaka juzi Simba ilishinda bao 3-1 wakati mwaka jana walishinda 2-0.

Post a Comment

 
Top