BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF) limedaiwa kuwa lipo kwenye mchakato wa kumnasa aliyekuwa kocha wa Toto Africans ya jijini Mwanza, Martin Grelics ambaye tayari alitangaza kujiuzulu kuifundisha timu hiyo.Habari kutoka ndani ya TFF zinasema kuwa endapo mabosi hao wa soka nchini watafanikiwa kumnasa kocha huyo basi atakabidhiwa timu ya vijana walio na umri chini ya miaka 15 ambayo kwasasa inafundishwa na kocha mzawa Bakari Shime.

Chanzo hicho kimesema kuwa tayari maofisa wa TFF wamekabidhi jina hilo kwa Rais wao Jamal Malinzi ambaye analifanyia kazi ingawa imeelezwa kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kumpata.

''Martin ni kocha mzuri na tumeona anafaa kwenye timu yetu ya vijana. Tumempelekea Rais hilo jina ili alipitie na kama ataridhishwa nalo na kiwango alichokionyesha kwa mechi chache za Toto basi utafanyika mchakato wa kumpa ajira,'' alisema kiongozi huyo

Martin alijiuzulu kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kushindwa kuendana na mfumo wa viongozi wake wa Toto Africans ambao ulikuwa unampa wakati mgumu katika kutekeleza majukumu yake.

Post a Comment

 
Top