BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
INAWEZEKANA ni homa ya pambano la leo kati ya Taifa Stars na Algeria iliyosababisha Shirikisho la Soka nchini (TFF)badala ya kubandika picha ya straika Mbwana Samatta kumpongeza kwa kutwaa kiatu cha dhahabu walijikuta wanaweka picha ya Rainford Kalaba kwenye skrini ya Uwanja wa Taifa.

Picha ya Kalaba 


Samatta aliibuka Mfungaji Bora kwenye michuano ya Mabingwa wa Afrika kwa kufikisha mabao nane huku timu yake ya TP Mazembe ikitwaa ubingwa huo ikiwa ni mara yao ya tano.

Katika 'screen' hiyo TFF waliandika maneno ya kumpongeza Samatta huku picha ikiwekwa ya Kalaba pasipo kushitukia mpaka walipoamua kutoa na kuweka ubao wa kuonyesha  matokeo ikiwa ni dakika chache kabla ya mpira kuanza. Kalaba pia ni mchezaji wa Mazembe.

Katika mechi hiyo ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018, Stars ilitoka sare ya bao 2-2 na Algeria. Mabao ya Stars yalifungwa na Elius Maguli pamoja na Samatta.

Post a Comment

 
Top