BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF) limetoa kalenda ya dirisha la usajili kwa vilabu vya Ligi Kuu (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) lililofunguliwa Novemba 15, litafungwa Disemba 15 mwaka huu pamoja na muongozo wa jinsi ya kufanya usajili huo.Klabu zinazoshiriki ligi hizo zilizopo chini ya TFF zinaombwa kufanya usajili katika muda uliopangwa ili kuepuka kuchelewa na kufungwa kwa dirisha hilo.

Usajili wa dirisha dogo ni kwa klabu  ambazo hazijajaza idadi ya wachezaji 30 katika usajili uliofanyika wakati wa dirisha kubwa la usajili (Juni – Agosti 2015), usajili huo wa wachezaji unafanyika katika tovuti ya TFF, www.tff.or.tz kisha kwenye link ya Club Registration.

Post a Comment

 
Top