BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
MBEYA City imempa mkataba wa mwaka mmoja beki wa kati Tumba Sued ambaye ataziba pengo la Juma Nyosso anayetumikia kifungo cha miaka miwili bila kucheza soka kutokana na kosa la udhalilishaji.

Nyosso alifungiwa na Shirikisho la Soka nchini (TFF)  baada ya kumfanyia vitendo vya utovu wa nidhamu straika wa Azam Fc, John Bocco.

Katibu Mkuu wa City, Emmanuel Kimbe amesema kuwa Sued ambaye alikuwa akikipiga Coastal Union ya jijini Tanga amemwaga wino wa kuichezea timu yao kwa mwaka mmoja na nusu.


Habari zaidi kutoka ndani zinasema kuwa Mbeya City wapo kwenye mipango ya kumrejesha beki mwingine Deo Julius aliyeachana na timu hiyo msimu uliopita na kujiunga na Kagera Sugar na imeelezwa kuwa Deo huenda akasaini mkataba na City muda wowote wiki hii.

''Amesaini mwaka mmoja na nusu bado tunaendelea kuboresha kikosi chetu kulingana na mahitaji aliyopendekeza kocha,'' alisema Kimbe

Kuhusu kipa Juma Kaseja alisema kuwa ''Tunazungumza naye ili kuona ni jinsi gani tutamwongeza mkataba kwani naye bado tunahitaji huduma yake na pia benchi la ufundi limetutaka kufanya jitihada za kumpa mkataba huo,'' 

Kaseja alisaini mkataba wa miezi sita ambapo kipindi hiki yupo huru kufanya mazungumzo na timu yoyote itakayomuhitaji.

Post a Comment

 
Top