BOIPLUS SPORTS BLOG

MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ Ester Chaburuma ‘Lunyamila’ ataagwa rasmi katika mchezo wa kirafiki kati ya timu ya Twiga Stars dhidi ya timu ya taifa ya wanawake ya Malawi utakaochezwa  Jumamosi katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

Chaburuma amekuwa ni miongoni mwa wachezaji waanzilishi wa Twiga Stars ambapo amekuwa akiitumikia timu hiyo tangu kuanzishwa kwake mpaka sasa timu inapojiandaa na mchezo dhidi ya Malawi.


Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake ya TFF, Amina Karuma amesema wameamua kutumia mchezo huo wa kirafiki kwa ajili ya kumuaga Chabruma ambaye amekuwa ni chachu ya maendeleo ya mpira wa miguu kwa wanawake, kutokana na kuwafanya wanawake wengi kujitokeza kucheza mchezo huo.

Naye kocha wa timu hiyo, Rogasian Kaijage amesema vijana wake wapo vizuri na wanaendelea na maandalizi ya mchezo huo ambapo anaimani watautumia vizuri katika kumuaga mchezaji mwenzao wa siku nyingi ambaye anastaafu kucheza soka.

Post a Comment

 
Top