BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Christian Simba
HATIMAYE Bondia Tyson Fury ametawazwa kuwa  bingwa mpya wa ndondi za kulipwa uzito wa juu, baada ya kumpiga Wladimir Klitschko katika pambano kali la kihistoria liliofanyika Dusseldorf Ujerumani.


Tyson amemshinda Klitschko wa Ukraine kwa pointi huku majaji wawili wakimpa ushindi wa pointi 115-112 na jaji mwingine akimpa ushindi wa pointi 116-111  Tyson fury mwenye  umri wa miaka 27 anabeba mataji yote makubwa ya ngumi uzito wa juu, WBA, IBF na WBO.

Katika pambano hilo Fury alionekana kuwa amejipanga vilivyo  hakumpa nafasi Klitschko ya kutamba ulingoni na kumrushia  makonde mfululizo akitumia mikono na mitindo yote kiasi cha 'kumharibu sura' mpinzani wake hiyo.


Klitschko ameahidi kutakuwa na mchezo wa marudiano baada ya kupoteza pambano hilo inaaminika kuwa katika mkataba waliiokubaliana kuwa kuliku na kipengele cha kupata mechi ya marudiano klitschko amesema.

Hili ni pambano la kwanza kupoteza kwa Klitschiko toka mwaka 2004 na rekodi yake imebaki kuwa ameshinda mapambano 64 na kupigwa 4


Post a Comment

 
Top