BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga wamedaiwa kuanza kumnyatia kinara wa mabao Elius Mafuli ambaye amefikisha idadi ya mabao tisa mpaka sasa wakitaka kumsajili kwenye dirisha dogo la usajili ambalo limefunguliwa rasmi leo.

Maguli ambaye anaichezea Stand United ya Shinyanga akitokea Simba ambao walimuacha kutokana na mapendekezo ya kocha wao Dylan Kerr ambaye hakuridhishwa na kiwango chake wakati timu hiyo ikiwa kwenye maandalizi ya ligi msimu huu.


Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam zinasema kuwa wakongwe hao kuwa wamevutiwa na kiwango cha Maguli na kwamba anaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa lakini usajili wake ni lazima ufuate taratibu zote za usajili.

Hata hivyo Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tibohora amesema kuwa ''Ni kweli mchezaji kama Maguli anaweza kutusaidia ila ni mchezaji  halali wa Stand hivyo ni lazima zifuatwe taratibu na hatuwezi kukurupuka kufanya usajili bila kufuata utaratibu kwani Yanga ni timu kubwa.

''Lakini kama Maguli mwenyewe atakuwa tayari kuvunja mkataba wake basi tunaweza kufanya hivyo lakini sisi bado tuna wachezaji wazuri hata kama hatuwezi kumpata Maguli,'' alisema Tibohora.

Jana Maguli aliisaidia Taifa Stars kupata sare ya bao 2-2 dhidi ya Algeria huku bao lingine likifungwa na Mbwana Samatta ambaye ni Mfungaji Bora wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika. Stars ilitoka sare kwenye mechi hiyo ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018.

Post a Comment

 
Top