BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Akram Msangi 'Mido'
YANGA leo imeendeleza ubabe katika mechi zake za kirafiki kwa kuifunga timu ya Shule ya Sekondari ya Makongo mabao 3-0, mechi hiyo imechezwa Uwanja wa Boko Veteran, jijini Dar es Salaam.Yanga ilipata bao lake la kwanza dakika ya tano kwa mkwaju wa penalt ambayo ilipigwa na kipa Deogratius Munishi 'Dida' baada ya mabeki wa Makongo kumchezea rafu Frank Gerald.

Yanga waliendendelea kulishambulia lango la wapinzani wao ambapo dakika ya 14, James Msuva alipiga krosi dongo iliyomshinda kipa wa  Makongo na kumkuta Gerald aliyeuzamisha mpira wavuni kwa utulivu mkubwa. Baada ya kufungwa goli la pili, Kocha wa makongo aliwaita vijana wake na kuwatuliza ambapo walirudi kwa utulivu na umakini mkubwa na kufanikiwa kufanya mashambulizi mfululizo langoni mwa Yanga lakini ukuta wa Yanga ulioongozwa na  Mbuyu Twite pamoja na Thaban Kamusoko ulikuwa makini kuokoa hatari hizo.

Dakika ya 41 Straika, Donald Ngoma aliandikia bao la tatu baada ya kugongeana vema na Msuva na kuifanya Yanga iende kupumzika ikiongoza bao 3-0 bao ambazo hazikuweza kusawazishwa wala kuongezwa mpaka dakika 90 za mchezo huo kumalizika.

Post a Comment

 
Top