BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally, Blida, Algeria
KATIKA kile kiliichoonekana kama ni kutaka kuiwekea vizingiti Taifa Stars katika mechi yao ya marudiano  itakayochezwa usiku wa leo wenyeji Algeria waliilalamikia rangi ya jezi ya kipa Ally Mustafa ambayo ataitumia kwenye mchezo huo kuwa inafanana na rangi ya jezi ya kipa wao.


Hayo waliyalalamikia katika kikao cha leo kuelekea kwenye mchezo huo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018 ambapo Algeria waliweka pingamizi kipa huyo asitumie jezi yenye rangi hiyo na kwamba Stars wasivae jezi zenye rangi nyeupe wanazotumia ugenini.

"Walitaka Stars ibadili rangi ya jezi na sisi tuliwaambia hilo haliwezekani kwa kuwa jezi ya rangi nyeupe ndio jezi rasmi ya Stars ikicheza ugenini. FIFA iliamua tutumie jezi hiyo na wao kipa wao abadili tayari kwa mchezo huo.

"Tumeshukuru FIFA kuhusishwa kwa kuamini kuwa mechi yetu itakuwa katika uangalizi ili kuepuka hujuma na uonevu wakati wa mechi,'' alisema kiongozi huyo.

Kikao hicho cha maandalizi ya mechi kilifanyika Mji mkuu wa Algiers uliopo takriban kilomita 50 kutoka Mkoa wa Blida ambako mechi hiyo itachezwa  katika Uwanja wa Mustapha Tchaker.

Post a Comment

 
Top