BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
KLABU ya soka ya Acacia Stand United ya mjini Shinyanga  imefanikiwa kunasa saini ya beki  kutoka nchini Ivory coast, Assouman N'guessan David ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili akitokea timu ya Olympique Sports Abobo FC (FC.OSA).Akizungumza na BOIPLUS, Msemaji wa timu hiyo Deo Kaji Makomba amesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ameingia mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo inayosika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu, wakiamini kuwa atakuwa na msaada mkubwa kwao na kuziba pengo la Hamad Ndikumana ambaye ametemwa.

''Haya ni mapendekezo ya kocha mkuu wetu, Patrick Leiwig, wakati huu wa dirisha dogo la usajili, lakini pia tupo mbioni kupata wachezaji wengine wawili wa hapa hapa nyumbani Tanzania,'' alisema Makomba maarufu kama Simple Man.

Acacia Stand United ipo katika mikakati mikubwa ya kuimarisha kikosi hicho ambapo wachezaji wawili wazawa watasajiliwa muda wowote kuanzia sasa mmoja ni mchezaji huru huku mwingine akitokea klabu kubwa hapa nchini ambaye wanamchukuwa kwa mkopo.

Post a Comment

 
Top