BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
UONGOZI wa timu ya Acacia Stand United ya Shinyanga umetangaza wachezaji waliowatema huku wengine wakipelekwa kwa mkopo katika timu mbalimbali lakini mchezaji Hassan Dilunga aliyesaini mkataba wa miezi sita kuichezea JKT Ruvu na kusisitiza kuwa mchezaji huyo ni mali yao.

Waliotemwa ni Hamad Ndikumana, 
Hamad Manzi na Shaban Dunia huku waliopelekwa kwa mkopo ni Jisendi Mathias na John Mwenda wameenda timu ya Ligi Daraja la Kwanza ya Geita Gold, Heri Khalifa, Khalid Suleiman na Rashid Magona ambao wamepelekwa Polisi Tabora.Msemaji wa Accacia Stand United, Deo Makomba amesema kuwa tayari majina ya wachezaji hao yamepelekwa TFF kwa mujibu wa kanuni za usajili huku wakitarajia kupeleka kikosi kizima ambacho kitaendelea na mechi za Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu.

''Hao ndiyo tuliowaacha na wengine wamepelekwa kwa mkopo kwenye timu za FDL tutakapomaliza masuala ya usajili basi majina yote tutayapeleka TFF likiwemo jina la Dilunga ambaye ni mchezaji wetu halali,  ndiyo maana kwenye orodha ya wachezaji walioachwa yeye hayumo,'' alisema Makomba.

Post a Comment

 
Top