BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
KIPA aliyetemwa Yanga, Mudathir Khamis leo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Mgambo JKT ya jijini Tanga.

Mudathir alisajiliwa na Yanga mwanzoni mwa msimu huu akitokea KMKM ya Zanzibar lakini alishindwa kuendelea kuwemo kwenye kikosi cha Hans Pluijm kutokana na kutoridhishwa kwa kiwango chake.Pluijm aliutaka uongozi kuvunja mkataba na kipa huyo ambaye hakuwahi kucheza hata mechi moja kati ya tisa walizocheza kabla ya kwenda mapumziko ambapo alikuwa akiishia kukaa jukwaani.

Mudhathir amethibitisha kusaini mkataba na Wanajeshi hao akiamini kwamba hapo ni mahali sahihi ambapo anaweza kuonyesha kiwango chake.

Akiwa Yanga, kipa hiyo alikuwa anakutana na upinzani mkubwa kutoka kwa makipa watatu Ally Mustafa 'Barthez', Deogratius Munishi 'Dida' na Benedicto Tinocco

Post a Comment

 
Top