BOIPLUS SPORTS BLOG

MASHABIKI wa Arsenal watakuwa ni wenye furaha kubwa wikiendi hii baada ya timu yao kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Aston Villa, huku matokeo ya mchezo huo uliopigwa Villa Park ukiwapeleka kileleni washika bunduki hao.


Mshambuliaji Olivier Giroud aliipatia Arsenal bao la mapema katika dakika ya nane tu ya mchezo kwa njia ya penati kabla Aaron Ramsey hajaiandikia Arsenal bao la pili akitumia vema pasi ya Mesut Ozil.


Arsenal imeshinda michezo 10 msimu huu na kuifanya ikae juu ya Manchester City kwa tofauti ya pointi moja huku Aston Villa wenyewe wakibaki na pointi sita tu katika michezo 16 iliyocheza.

Post a Comment

 
Top