BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Karim Boimanda
WASHIKA Bunduki wa Emirates, Arsenal, leo wameutumia vema uwanja wao wa nyumbani kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wageni wao Manchster City katika mchezo wa ligi kuu Uingereza.

Arsenal walijipatia bao lao la kwanza katika dakika ya 33 mfungaji akiwa Theo Walcott kwa shuti kali kufuatia pasi ya Mesut Ozil


Dakika moja kabla ya mapumziko, Ozil alifanya kazi ya ziada, safari hii akimtengenezea Olivier Giroud aliyefunga kwa mguu wake wa kushoto na kuifanya Arsenal iende mapumziko wakiwa kifua mbele.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu lakini mashambulizi hayo hayakuzaa matunda hasa ķutokana na uimara wa walinzi wa timu zote mbili.Yaya Toure aliwafuta machozi Man City kwa bao zuri la dakika ya 82 akimalizia kazi nzuri ya Bacary Sagna na kufanya mchezo huo umalizike kwa Arsenal kuibuka wababe kwa mabao 2-1.

Kwa matokeo hayo, Arsenal inaendelea kutesa katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na Leicester City huku Man City wenyewe wakibakia nafasi ya tatu

Post a Comment

 
Top