BOIPLUS SPORTS BLOG

Na Sheila Ally
AZAM FC leo wamecheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mgambo Shooting na kulazimisha sare ya bao 1-1, mechi ambayo imechezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Mechi hiyo ni moja ya maandalizi kuelekea mechi za Ligi Kuu Bara ambapo Desemba 12 Azam watacheza na Simba katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Azam ndiyo walikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za Maafande hao kupitia kwa mshambuliaji wao Kipre Tchetche aliyefunga bao hilo dakika ya 13 huku straika wa Mgambo, Fully Maganga akisawazisha bao hilo kipindi cha pili dakika ya 87.

Azam wanatarajia kucheza mechi nyingine keshokutwa Jumamosi dhidi ya African Sports ambayo pia ni ya Ligi Kuu na watarejea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya kucheza na Simba.


Azam ndiyo wanaongoza ligi wakiwa na pointi 25 huku mabingwa watetezi Yanga wakishika nafasi ya pili kwa pointi 23, Mtibwa Sugar wana pointi 22 wakati Simba wao wanashika nafasi ya nne kwa pointi 21.

Post a Comment

 
Top